Young Dee- Nataka Kumsaini Young Killer

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vyema katika ulimwengu wa kuchana Young Dee aka Paka Rapa amefungukia mipango yake kumsaini msanii mwenzake Young killer Msodoki.

Kwa mara ya kwanza Young Dee aliweka wazi mipango yake ya kumsaini Young Killer kwenye label ya King cash ambayo anafanya nayo kazi kwa sasa na  kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

download latest music    

Hahaha siku ya kwanza ofisini wakati nataka kumsign mdogo wangu #youngkillermsodokii?? ni kweli anachana sana kijana ana kipaji!”.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Young Dee alifunguka na kumwagia sifa kibao msanii huyo ambapo aliandika:

Young Killer ni rapa mzuri sana, namkubali sana lakini ishu za kumsaini ni mapema sana pale niliandika kama masihara lakini mimi nadhani ni jambo ambalo linawezekana kama nikiamua kwa sasabu ana kila kitu”.

Hivi sasa Young Killer Msodoki anafanya  kazi chini ya label ya Wanene Entertainment.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.