Young Dee- Nimeiga Wimbo Wa Mr. Nice Kwa Heshima

Msanii wa Bongo fleva Young Dee ameibuka na kudai kuwa kitendo cha yeye kuiga wimbo msanii mkongwe wa Bongo fleva Lucas Mkenda maarufu kama Mr.Nice Ilikuwa ni kwa sababu ya heshima aliyonayo kwenye mziki wake na wala sio wizi.

Baada ya Young Dee kutoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Kiben10 ambao ndani yake ameweka kionjo cha wimbo wa Mr.Nice bila ruhusa, ndipo pale jasho lilimtoka kwani Mr. Nice alipousikia wimbo huo alimjia juu Young Dee kwenye mitandao ya kijamii na kudiriki kumuita mwizi wa kazi zake na kutishia kumchukulia hatua za kisheria.

download latest music    

Young Dee amemjibu Mr. Nice na amejitetea kuwa yeye kuimba wimbo wake haikuwa kwa nia mbaya bali alifnya vile kwa sababu alikuwa shabiki Mkubwa wa wimbo wa Mr. Nice.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitua kipindi Chao cha Enews Young Dee alifunguka:

Naomba niseme kuwa sikuwa na nia mbaya bali nia yangu ilikuwa ni kumpa heshima maana hawa ni kaka yangu aliyenitangulia katika gemu alafu ana mchango mkubwa kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo lengi langi lilikuwq ni kumuonyesha heshima aliyoiweka kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kiasi ya kwamba miaka mingi baada ya wimbo huo kuhit lakini bado Una ladha ya kipekee kabisa”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.