Young Dee Yuko Tayari Kwenda Mahakamani Kisa Meneja Wake

Msanii wa hip- hop nchi Young Dee amefunguka na kusema kuwa tangu ametoa wimbo wake wa naoa anafaya kazi yeye mwenyewe  bila kuwa na uongozi wowote kwa sababu alishaachana na uongozi uliokuwa ukimuongoza hapo awali.

Young dee ambae alitangaza kuwa kwa sasa anafungua kampuni yake mwenyewe hivyo kila kitu anachofanya atakuwa akisimamia yeye mwenyewe,.

download latest music    

Hata hivyo alikuwa akiongea na eNEws ta EATV ,YoungDee aliulizwa kuhusu swala la meneja wake huyo anaejulikana kwa jina la Sudi kutaka kwenda kumgungulia mashtaka kwa kile kinachodaiwa kuwa amevunja mkataba bila kufuata makubaliano yao.

Baada ya kuulizwa Young Dee alisema kuwa hata yeye yuko tayari kwenda mahakamni kwa sababu ya swala hilo kwa sababu anachojua ni kwamba walishamalizana siku nyingi.

Mimi nilishafuta kila kitu kisheria na  kuhusu mkataba kama anataka  kufanya chochote afate sheria maana mimi niko tayari hata kwenda mahakamani.

Young dee anasema kuwa alikuwa na malengo aliyokuwa amejiwekea lakini ilifika muda akaona kuwa itakuwa ngumu kuyafanikisha na kwa sababu yeye ni mwanaume na ana majukumu hakuona sababu ya kukaa hapo zaidi ya kupambana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.