Young Killer Afunguka Baada Ya Aliyekuwa Mpenzi Wake Kushika Ujauzito Wa Mwanaume Mwingine

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Killer amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya habari kusambaa kuwa aliyekuwa mpenzi wake Halimaty au maarufu kama Miss Hip hop amebeba ujauzito wa njema nyingine.

Young Killer na Miss Hip Hop walikuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini Habari za wawili hao kuachana zilisambaa wiki chache zilizopita.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Soudy Brown Kupitia Clouds Fm Young Killer amesema hajakasirikia wala kuona wivu kuona Ex wake amebeba ujauzito wa mwanaume mwingine kwani ni jambo la kawaida.

Ni jambo la kheri, hapana siumii kwa sababu hakuna kitu kama kuona mtu ambaye mlikuwa mnapeana furaha anaendelea kufurahi”.

Lakini pia Young Killer amekanusha taarifa kuwa kipindi cha mahusiano yao alikuwa akimnyanyasa mrembo huyo.

Hapana, ni maneno ya watu hayo kwa sababu matatizo madogo madogo, sijui michepuko huwa ni vitu vya kawaida kwenye mapenzi, huwa havikosi, umenisoma?”.

Hivi sasa Young Killer anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa Shots aliomshirikisha Khaligraph Jones kutoka Kenya.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.