Z Anto kumshirikisha mwanawe wa umri wa mwaka 1 kwenye kazi yake mpya

Msanii Z Anto ambaye amekuwa kimya kwa muda sasa ameweza kufunguka kuhusu project yake mpya ambayo ataiwachia hivi karibuni.

download latest music    

Z Anto akizungumza na Bongo5 wakati wa show ya Hweshima ya Bongo Flava, iliyoandaliwa na EATV, alisema kuwa kwa hivi sasa anajitayarisha kuachai nyimbo mpya ambayo amemshirikisha mwane mwenye umri wa mwaka mmoja.

Hata hivyo kwa mara ya kwanza Z Anto alisema kuwa yeye hategemei mziki kupata hela kwani ananjia zingine anazozitumia kupata mkwanja. Z Anto aliambia Bongo 5,

“Sikuwa nategemea sana muziki katika maisha yangu. Hizi ni biashara za familia yangu ndio maana. Hata hivyo sio kiki kuwa hizo fremu ni zangu.”

Tazama interview hiyo hapa:

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua