Zabibu Kiba Afunguka Mahusiano Yake na Jokate.

DADA wa mwana-muziki maarufu Bongo, Ally Salehe Kiba ‘Ali- Kiba’, Zabibu amem-fungia mpenzi wa zamani wa kaka yake huyo ambaye ni mwanamitindo na mjasiriamali Jokate Mwegelo, na kusema kuwa hata kama hayupo ndani ya familia yao bado anamheshimu sana.

Akizungumza na Over Ze Weekend nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar hivi karibuni, Zabibu alisema kuwa, Jokate kwake ni kama dada yake na wala hana tatizo naye na wanazungumza naye vizuri kama ilivyokuwa zamani na pia anamheshimu kwa sababu ni binti anayejielewa.

download latest music    

Siwezi kuzungumzia kitu chochote kibaya kuhusiana na Jokate kwa sababu ni kama dada yangu kabisa ninamheshimu na ninampenda sana halafu pia tunaongea tu vizuri hatuna shida yoyote na ni msichana anayejielewa mno,” alisema Zabibu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.