Zabibu Kiba Asemekana Kuwa ni Mjamzito

Dada wa staa wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba, Zabibu Kiba amedaiwa kuwa wiki chache baada ya kufunga ndoa tayari Mrembo huyo amesha kikwaa kibendi na ni mjamzito.

Zabibu alifunga ndoa na mume wake Abdi Banda ambaye ni mcheza mpira wa kulipwa nchini Afrika ya Kusini mwezi uliopita na sasa kuna taarifa zinasema Zabibu anawezaakawa kashanasa ujauzito.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa kuna tetesi zilianza kusambaa baada ya Picha ya Zabibu kuanza kusambaa kupitia mtandao wake wa WhatsApp ambapo wapenda ubuyu waliichukua picha hiyo na kuanza kuijadili mitandaoni.

Picha hiyo iliyomuonyesha Zabibu akiwa kama mjamzito iliibua mijadala man kupelekea watu kuamini huenda Mrembo huyo tayari ameshabeba mimba.

Baada ya picha hiyo kuzua gumzo, mwishoni mwa wiki iliyopita Gazeti la Amani lilimtafuta mrembo huyo ambaye amehamishia makazi yake ya kudumu nchini Afrika Kusini kwa mumewe Abdi anayesakata kandanda nchini humo katika timu ya Baroka ambapo alipopatikana alikanusha madai hayo na kudai kuwa amenenepa tu.

Hahaha jamani sina kitumbo ni unene tu huu“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.