Zamaradi Mketema Akana Kabisa Kuajiriwa Wasafi Tv

Mtangazaji na Mdau mkubwa wa tasnia ya Bongo movie Zamaradi Mketema ameibuka na kukataa kata kata kuwa amewahi kuajiriwa na kituo cha televisheni cha Wasafi Tv.

Miezi michache iliyopita Baada ya Zamaradi kuachana rasmi na Clouds Media alikokuwa anafanya kazi kwa muda mrefu alianza kuonekana na Mkurugenzi wa Wasafi Tv Diamond Platnumz na kuaminika kuwa ataanza kufanya kazi katika kituo hiko.

download latest music    

Lakini sasa Zamaradi anakataa na kusema kuwa tofauti na watu wengi wanavyoamini yeye hajawahi kuajiriwa na Wasafi bali aliingia nao mkataba wa kufanya nao kazi kama mtu anayejitegemea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Zamaradi alifunguka hay kuhusu ishu yake ya kufanya kazi na Wasafi:

Kwani ni lini nilisema nipo Wasafi au sio huko Wasafi Tv ni partners tu na sijawahi kuajiriwa kokote na hii nilishawahi kuongea zaidi ya mara mia”.

Zamaradi alikana pia tetesi za kuwa amegombana na Diamond ndio maana mkataba Wake na Wasafi umevunjwa:

Sio kwamba tumeachana kuna project zipo zitakapokuwa tayari tutaendelea kufanya kazi kama kawaida kwahiyo siyo kwamba niliajiriwa  nikavunja mkataba au walikuwa wameniajiri wakanivunjia mkataba siajwahi kusaini mkataba na mtu yoyote wa ajira”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.