Zari Adaiwa Kumfanyia Zengwe Diamond

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Zarinah Hassan wamerudi Tena Kwenye headlines ambapo sasa inadaiwa Zari Kamfanyia Zengwe Diamond mpaka kuharibu Birthday ya Tiffah.

Global Publishers wanaripoti kuwa Diamond alitangaza  kuangusha bonge la sherehe nchini humo, Lakini sasa inadaiwa Zari amemfanyia zengwe Diamond kiasi cha kumfanya jamaa huyo anyooshe mikono na kuahirisha sherehe hiyo bila kupenda.

download latest music    

Unajua ile bethide Diamond alikuwa anaiandaa kwa ushirikiano na kampuni (anaitaja jina) na kampuni hii ndiyo ambayo inawadhamini Diamond na Zari katika mambo mbalimbali kwani kampuni hiyo nayo inanufaika pia kwa jinsi wawili hao wanavyoitangaza kupitia matangazo mbalimbali wanayoyaandaa. Sasa kulikuwepo makubaliano kwamba ili wadhamini hao waendelee kutoa fedha, Diamond na Zari wanapaswa kuposti sherehe hiyo katika akaunti zao za Instagram, sasa mwanzoni bidada Zari anaonekana alikubali, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda akapiga kimya tu”.

GPL wanazidi kuripoti kuwa kutokana na matukio yaliyokuwa yanaendelea kutokea Zari aligoma kabisa kushiriki kuiposti sherehe ile na badala yake alikuwa bize na mambo yake binafsi ikiwemo Shindano la Miss Uganda.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilimsaka Diamond bila mafanikio lakini Meneja wake Babu Tale alifunguka haya kuhusu sherehe ile:

Unajua hii ni pati, bethidei ya Tiffah ilishapita lakini nikwambie tu itafanyika na kutakuwa na sapraizi mtaona”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.