Zari Afungukia Magumu Aliopitia 2018 na Kuupokea 2019

Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka mwaka 2018 na kuupokea 2019.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake, Ivan.

download latest music    

Lakini Pia Zari alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujenga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia.  Anasema alijijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.   Asante, nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018“.

https://www.instagram.com/p/Br2SY6ln7KC/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=sy9rx7neaahn

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.