Zari Ajitapa Kuwa na Pesa Chafu Asisitiza Hawezi Kujibizana na Watu Mtandaoni

Zarinah Hassan au maarufu kama Zari The Bosslady amefunguka na kuweka wazi kuwa ana pesa nyingi kupita kiasi na kusema hawezi kujibizana na Watu mtandaoni.

Siku chache zilizopita Zari aliandika Mtandaoni kuwa yeye ni bilionea na kuwaita watoto wake matajiri, kauli iliyoibua maneno mengi mtandaoni ambapo watu wengi walimnanga na kudai hana pesa.

download latest music    

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Zari amesema anawashangaa watu wanamnanga na kuamua kuweka wazi mali zake na kutaja biashara zake anazofanya Afrika ya Kusini:

Kuna watu wengi sana hawajui maisha halisi ya Zari, wanakisia tu mitandaoni, Ninaandaa shoo yangu ya TV, ambayo inazungumzia maisha yangu halisi, nadhani wengi watamjua Zari halisi. Nina mambo mengi wasiyoyajua.

Hawajui hapa Afrika Kusini nimewekeza kiasi gani? Ivan aliacha mali kiasi gani? Haya natakiwa kuyaendeleza kwa ajili ya watoto wake. Yapo magari yake ya kifahari hata mimi siyaendeshi.

Tuna shule hapa Afrika Kusini, kampuni ya ulinzi, nimeajiri wafanyakai 360, kila mwisho wa mwezi nalipa mishahara yao. Siwezi kujibizana na mtu mitandaoni”.

Zari alijizolea umaarufu Bongo baada ya kuanzisha Mahusiano ya Kimapenzi na kuzaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.