Zari Amedai Kuwa Hawezi Kuzaa Tena na Diamond, Akitaka Akazae na Wanawake Wengine (video)

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’ amefunguka na kudai kuwa hawezi kuendelea kuzaa na mpenzi wake na mzazi mwenzake mwanamuziki Diamond Platnumz na akiona anahitaji watoto zaidi akazae na mwanamke mwingine.

Zari na Diamond walipoanza mahusiano yao kimapenzi miaka kama minne iliyopita walianza kwa kasi ya ajabu kwani mara tu baada ya kuwa pamoja kwa miezi michache Zari alibeba ujauzito na kujifungua mtoto wao wa kwanza Tiffah na miezi michache baadae alijifungua mtoto wao wa mwisho Nillan.

download latest music    

Miezi michache iliyopita Zari alipitia kipindi kigumu kwenye mahusiano yake na Diamond baada ya kugundua kazaa tena na mwanamke mwingine ambaye ni Hamisa jambo lililopelekea watu wengi kudhani ataachana na Diamond lakini wamesameheana na wapo wote pamoja.

Lakini pamoja na kwamba bado wapo wote Zari amesisitiza kuwa hawezi tena kuzaa na Diamond na kudai endapo atataka mtoto mwingine basi yupo huru kwenda kuzaa na wanawake wengine lakini sio yeye.

Zari alifunguka hayo yote kwenye mahojiano aliyofanya na Milard Ayo TV:

Kwa upande wangu mimi wametisha siwezi kuongeza wengine lakini kama Diamond anataka watoto wengine anaweza akawa nao wengi atakavyo hilo ni tatizo lake sio langu mimi Niko fresh tu”.

 Zari ambaye tayari ana watoto watatu wakubwa wa kiume aliozaa kwenye ndoa yake na Ivan kwaiyo kufanya jumla ya watoto watano alionao hivi sasa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.