Zari Amefunguka Mazito Kuhusu Usaliti Wa Diamond , Adai Kilichomkera Yeye Kulala na Hamisa Kitandani Kwao Bila Kinga

Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Diamond Platnumz, Zari the Boss lady amefunguka kuhusiana matatizo waliyopitia yeye na mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ miezi michache iliyopita baada ya Diamond kuzaa na Hamisa.

Miezi michache iliyopita habari hii ilienea kama moto wa kifuu na kusababisha tafrani kwenye mitandao ya kijamii pale Diamond alipoebda Clouds Fm na kukiri kuzaa na Hamisa na kumsaliti mpenzi wake Zari aliyezaa naye watoto wawili.

download latest music    

Baada ya sakata hilo Diamond na Zari walisameheana na kurudiana lakini tangu siku ile Zari hajawahi kuongelea ishu hiyo wala kueleza chochote kuhusu alivyojisikia mpaka juzi alipofanya mahojiano nchini Uganda.

Zari yupo nchini Uganda sasa hivi akijiandaa na tamasha lake analofanyaga la Zari All White Party litakalofanyika tarehe 21 nchini Uganda. Katika jitihada za kuitangaza shughuli hiyo anaputa kufanya interview na vituo mbali mbali vya redio.

Kwenye interview aliyofanya na ‘Celeb select’ Zari alifunguka mengi kuhusu uhusiano wake Diamond moja kati ya vitu alivyoongelea ni Diamond kuzaa na Hamisa na kumsaliti:

Diamond kutembea na kuzaa na mwanamke mwingine ni usaliti mkubwa sijapata kuona na kwa muda mrefu nilifikiri sitakuja kukaa na kuiongelea hii ishu lakini kwa kuwa ilishapita na nimeshapata amani kwaiyo haina shida. Unajua wanaume wengi wana-cheat lakini mimi kilichonitatiza ni kwa nini ulete mwanamke wako kitandani kwetu tunakolala wote? Kwanini utembee na mwanamke ambaye haeleweki wala hana thamani? Alafu kikubwa kwa nini haukuvaa kondomu na unajua kabisa tuna watoto wadogo na unaweza kupata ukimwi? Kusema kweli nilimuuliza maswali mengi na majibu yake yakawa na visingizio kibao mara ooh unajua wewe uko mbali ikatokea Bahati mbaya akabeba ujauzito wangu, nikasema sawa kwanini sasa ulimleta kitandani kwetu? Akasema unajua mimi ni maarufu sana ningeenda hotelini watu wangeniona kwaiyo inabidi aje usiku sana na kuondoka asubuhi sana ili watu wasimuone”.

Lakini Zari amesisitiza kuwa hawezi kumkataza Diamond kumuona mtoto wake aliyezaa na Hamisa kwani mtoto hana kosa lolote ni malaika tu. Pia amesema yeye na Diamond wako vizuri na amebadilika sana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.