Zari Amkumbuka Ivan Katika Siku Yake Ya Kuzaliwa

Mwanamama mjasiriamali na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amkumbuka Marehemu Ivan katika siku yake ya kuzaliwa.

download latest music    

Zari amemuandikia ujumbe mzito aliyekuwa mume Wake Ivan Semwanga ambaye alikufa mwaka jana kutokana na maradhi ya moyo.

Mbali tu ya kuwa alikuwa mumewe kwa miaka mingi Lakini pia ni baba wa watoto watatu wa kiume.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika maneno haya kama ishara ya kumkumbuka:

Leo ungetmiza umri wa miaka 41 kama ungekuwepo hai, lakini Mungu alikuwa na mipango yake mingine, ndio ingawa tunakukosa wewe kuwa hapa kimwili lakini nahisi kama hujaondoka upo na sisi. Ninakuona kupitia watoto wako, ninahisi uwepo wako kila mahali mimi nilipo, Urithi wako unaendelea kuishi, Endelea kulala kwa amani mpaka tutakapokutana tena.”

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.