Zari Ampa Za Uso Mwanaume Aliyetaka Kumuhonga Gari

Mwanamama mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amempa makavu ya Uso msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya Ringtone Apoko.

Tangu Zari aachane na Diamond Msanii huyo amekuwa akiyuka mtandao wa kijamii kueleza kuwa anampenda sana Zari na yupo tayari kwenda kutoa mahari Uganda ili amuoe.

download latest music    

Lakini wikiendi iliyopita aliibuka na jipya baada ya kusikia Zari anaenda Kenya aliwatuhumu ajili ya Tamasha kwani alidai ameamua kumnunulia gari aina ya Range Rover Sport ambalo alienda nalo mpaka kituo cha redio alipokuwepo lakini alimkosa.

Baada ya kumkosa Kwenye studio hizo Ringtone aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Zari akachukue zawadi yake hiyo aliyomnunulia.

Baada ya taarifa hizo kusambaa sana Kwenye mitandao ya kijamii Zari alifunguka Kwenye mahojiano na Kiss Fm na kusema hamfahamu mtu huyo na hajawahi kuwasiliana naye hivyo hawezi kupokea kitu chochote kutoka kwake:

Simfahamu huyo Ringtone na sijawahi kukutana naye, ndio mara ya kwanza kusikia kitu kama hicho. Nina watu zaidi ya milioni 3.9 katika mtandao wa Instagram ambao wananifuatilia, siwezi kujua nani kunifuata na kwa wakati upi”.

Lakini pia Zari aliweka wazi kuwa hana shida ya Range Rover maana wiki iliyopita ametoka kujinunulia Range Rover Sport mpyaa hivyo yuko vizuri.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.