Zari ‘Amtosa’ Diamond na familia Yake Yote Mtandaoni

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘ Zari’ ambaye ni maarufu Tanzania kwa kuzaa na uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameamua kumtosa Diamond na familia yake yote huko kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki hizi chache zimekuwa zikimhusisha mrembo Zari na mpenzi wake Diamond kwenye vichwa vya habari kila siku huku kila uchao ni stori mpya na mwanamke mwingine huku wiki hii ni Tunda ndiye anatawala headlines.

download latest music    

Kumekuwa na stori kwenye mitandao ya kijamii kuwa Tunda anatoka na Diamond lakini pia kikubwa ni kwamba ni baba wa mtoto wa Tunda aliye tumboni.

Piano kumekuwa na video clip inayomuonyesha msichana anayeitwa Mia ambaye ana undugu na Tunda huyu alipata umaarufu juzi juzi baada ya video yake kusambaa akiwa Nyumbani kwa Diamond Madale lakini baadae time ya Diamond ilidai msichana yule alikuwa demu wa dancer wa Diamond ingawa baadae alikuja sema kuwa alilala naye.

Lakini pia Diamond ana skendo nyingine kubwa ni kuwa yeye na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu wamerudiana hiyo imeonekana mwishoni mwa wiki iliyopita pale Wema na Diamond walipoanza kushikana shikana na kukumbatiana ukumbini halo iliyozua tafrani.

Baada ya skendo zote hizi kumfikia Zari ambaye hivi sasa yupo nchini South Africa ameamua kuwa-unfollow kwenye mtandao wa Instagram familia nzima ya Diamond kuanzia Diamond mwenyewe, Mama Diamond, Esma, Rommy Jones mpaka mameneja wote wa Diamond na Time nzima ya WCB.

Mara ya mwisho Diamond kuhojiwa nchini Rwanda alidai kuwa hana msichana mwingine zaidi ya Zari na bado wako wote hadi hivi sasa lakini Zari hajaongelea lolote kuhusu status ya relationship yao mpaka hivi sasa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.