Zari Amwaga Povu Zito Baada Ya Kukosolewa Kwa Vazi Lake

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka na kuwamwagia Povu zito watu waliomponda Baada ya kuposti picha ya utata.

Siku chache zilizopita Zari aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram zilizomuonyesha akiwa amevaa mavazi ya ndani ‘Swimming costume’ na kupelekea watu kumrushia maneno.

download latest music    

Mashabiki walimjia juu Zari na kumtuhumu kwa Kiba nusu uchi na kuanika kwenye mitandao ya kijamii ilhali akiwa ni mama  wa watoto watano na huku watoto wengine wakiwa wakubwa kabisa.

Baada yapovu hilo la mashabiki Zari aliibuka na kuposti kipande cha video kujibu mashambulizi na kwa sababu asilimia kubwa waliokuwa wakimchamba ni Wabongo, akaona naye bora awachambe kwa Lugha ya Kishwahili.

Jamani nikitaka kuvaa swimming cost kwa swim­ming pool hiyo ni maisha yangu, ukitaka kuvaa dera hiyo ni maisha yako usini­pangie maisha vile mimi sikupangii maisha naomba tuheshimiane, samahani”.

Zari alivaa mavazi hayo pembezoni mwa bwawa la kuogelea ambapo Hivi sasa yupo nchini Uganda na familia yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.