Zari apigwa vita kwa maazimio yake ya kutaka kurithi mali ya aliyekua mumewe

Familia na marafiki wa Ivan Ssemwanga tayari wanampiga vita Zari Hassan kwa maazimio yake ya kutaka kurithi mali ya aliyekua mumewe.

Matukio haya yaliwekwa wazi na Big Eye ya Uganda ambayo ilimhoji mmoja wa marafiki wa Ivan. Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Zari amevutana sana na Lawrence Kiyingi maarufu kama King Lawrence ambaye alitaka kupora mali ya Ivan.

download latest music    

King Lawrence ni mwandani wa Ivan na pia ni mwanachama wa kundi la Rich Gang ambayo ni maarufu sana nchini Uganda kwa kuhost parties za nguvu.

Rich Gang: King Lawrence (kushoto) na Ivan Ssemwanga (katikati)

Chanzo hicho kilieleza kuwa Zari and King Lawrence walitimuliwa hospitalini alipolazwa Ivan kwasababu walizua rabsha wakigombana kuhusu mali ya Ivan.

“At one point, these fights reached hospital and the two together with other family members had to be thrown out of hospital for the peace and sanity of the sick person. Ivan saw these fights, read some on Facebook but he just could not reply to anything. Someone had to hold the phone for him. And he had no reply just the hissing sounds. Deep down, he must have felt betrayed, used and abandoned by those he considered his closest,” Chanzo hicho kilisema.

Zari alionekana kwa video Instagram akigombana huku alisema kuwa mali ya mumewe wa kitambo ni ya watoto wake watatu aliyowazaa kama bado ni mke wa Ivan. Hii ilikua siku moja kabla ya Ivan kuaga dunia.

Zari na wanawe

Chanzo hicho pia kilisema kuwa Zari aliwaomba madaktari kuhairisha kutangaza kifo cha Ivan ili aweze kujipanga kable ya wanaomdulumu kuiba mali ya mume wake wa kitambo.

Mrembo huyo alitangaza mwenyewe kifo cha mumewe leo asubuhi baada ya kumaliza alichokuwa akifanya. Inasemekana Ivan aliaga dunia Jumanne asubuhi baada ya madaktari kudhibitisha kuwa viongo vyake kwa mwili vilifeli kufanya kazi.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere