Zari asherekea ushindi wa Rayvanny

Rayvanny aliwasili Dar jana kutoka Marekani ambapo alituzwa katika tuzo la BET. Muimbaji huyo alishinda katika kitengo cha Best International Viewers Choice Award.

Zari, ambaye hakua amesema lolote kuhusu ushindi wa Rayvanny, alisherekea ushindi wa Ray kwa kumpongeza kwa kupeleka Afrika Mashariki katika kiwango kingine

download latest music    

“Traffic imepunguka? We are so proud of you, you took East Africa and Africa in general on another level regarding the music industry. Be blessed @rayvanny cc @diamonplatnumz the Godfather of @wcb_wasafi where hits? are made,” Zari aliandika.

Wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki walimpongeza Rayvanny kwa ushindi wake. Jua Cali kutoka Kenya alisema ushindi wa Rayvanny unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.

“Unajua dream yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua competition ziko nyingi sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe and the moment kuna msanii wetu anashiunda tuzo kama hiyo, kwa sababu hiko ni kitu kikubwa sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri especially kwanza kiswahili. Unajua mimi ni mtu wa wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana,” Jua Cali alisema akiwa katika Citizen Radio.

Jua Cali

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere