Zari na Diamond Waibua Tetesi za Kurudisha Penzi Lao

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mama watoto wake Zarinah Hassan wamerudi tena Kwenye headlines za kurudiana.

Zari na Diamond waliachana mapema mwaka huu baada ya Zari kumwaga Diamond Kupitia post yake ya Instagram katika siku ya wapendanao.

download latest music    

Tangu waachane Zari amekuwa muwazi kuhusu Mahusiano hayo huku akiweka wazi kuwa aliumizwa na vitendo vya kudhalilishwa na Diamond baada ya kutuhumiwa kuwa Kwenye Mahusiano na warembo kibao huku Diamond amekuwa mgumu kuongelea uhusiano huo.

Lakini sasa kuna Tetesi zinazoendelea kuvuma Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zari ameamua Kurudisha majeshi kwa Baby dady wake baada ya Meneja wa Diamond Babu Tale kusafiri kwenda South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha.

Siku ya jana kuna clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Diamond akitua nchini South Africa lakini haijajulikana kama alifikia nyumbani kwa Zari au hotelini lakini Zari aliposti picha ya zawadi alinunuliwa na ‘Baba Nee’ ambaye anaweza kuwa Baba Nillan (Diamond).

Ingawa wawili hao hawajathibitisha taarifa za kurudiana lakini Dada wa Diamond Esma amedokeza hilo na kumposti Zari huku akidai yule ndio wifi yake wa ukweli.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.