Zari: Wema Amevuruga Penzi langu na Diamond

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Zarinah Hasssan ‘Zari the Bosslady’ amerudi tena kwenye headlines mwishoni mwa wiki hii baada kufanya Interview kwa mara ya kwanza baada ya kutangaza kumuacha Diamond rasmi.

Siku ya Valentine’s Zari aliushangaza uma wa watu baada ya kutangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ameamua kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake kwa kile alichodai ni michepuko imesababisha.

download latest music    

Lakini Zari ametaja sababu kubwa ambayo imepelekea yeye kuachana na Diamond ni mpenzi wake wa zamani (Ex wake) Wema Sepetu.

Wiki chache zilizopita video na picha zilizomuonyesha Wema na Diamond wakikumbatiana na kushikana hadharani kwenye party ya WCB.

Zari amefunguka mengi Kwenye mahojiano aliyofanya na BBC Swahili nchini Uingereza, London ambapo ameweka wazi alifikia uamuzi wa kumuacha Diamond baada ya kuona picha na video akiwa anakumbatiana na Wema Sepetu kusambaa kila kona Kwenye mitandao ya kijamii:

Kwanza hakuwa ametegemea mimi kuposti vile Instagram kutangaza kumuacha kwa sababu nilikaa mwenyewe muda mrefu nikafikiria mwishowe nikaamua tuishie hivyo”.

Zari amezidi kufunguka na kueleza kuwa walikuwa katika jitihada za kuuweka uhusiano wao kwenye mstari ulionyooka baada ya usaliti aliomfanyia uliompelekea kuzaa na Hamisa lakini alimuumiza zaidi alivyoona video akiwa anakumbatiana na Wema kwenye mitandao ya kijamii.

Unakaa leo unasikia hiki kesho unasikia kile kukumbatiana na ma-EX kwenye public kufanya vitu vya kunidhalilisha mimi na watoto wangu na unaona kabisa sio sawa na mtu ukiamua kuwa na familia unatakiwa vitu vingine unataka kama nimeshakukubali kuwa wewe ni msanii kutakuwa kuna vitu vingine unafanya lakini kuna vitu unatakiwa uweke stop ili kuiheshimu familia yako”.

Zari amefunguka na kusema baada ya kuona Diamond anapiga picha anakumbatiana na Wema kwenye social media aliamua kumblock kila sehemu hivyo alikuwa hana mawasiliano naye ya aina yoyote kuanzia hapo mpaka siku ya Valentines alipoamua kumuacha.

Zari amefunguka na kusema tangu amuache Diamond Kwenye Instagram hajawahi kuongea naye Tena wala kuwasiliana naye wala hajawaona watoto wao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.