Abdu Kiba: Tunda Alikuwa Mpenzi Wangu, Nimemiss”.

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Jeraha’ Abdu Kiba ambaye pia ni kaka wa Staa wa Bongo fleva Ali Kiba, amefunguka na kusema aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mrembo Tunda Sebastian.

Tunda ni video queen lakini pia ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ya Msanii Diamond Platnumz. Tunda alijipatia umaarufu wiki chache zilizopita baada ya tetesi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond lakini pia alizidi kupata umaarufu baada ya vieeo zake na Kinje kuvuja mtandaoni.

download latest music    

Ikiwa tunasherekea mwezi wa mapenzi ambapo juzi tu ilikuwa ni siku ya Wapendanao, Abdu Kiba alifunguka kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv ambapo alidai kuwa alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Tunda na yalikuwa matamu kiasi ya kwamba alitamani yasivunjike.

Kwenye interview hiyo aliyofanya siku ya Valentine’s Day Abdu Kiba alizidi kufunguka:

Mahusiano ambayo yaliwahi kunifurahisha ambayo sikutamani hata yavunjike long time ago lakini kipindi hiko nipo na Tunda ambapo tulikutana kupitia social media nilimwelewa na vile vile alinielewa kwaiyo tukaweza kukutana na mwishowe wote tukaelewana ila muda kidogo kama miaka mitatu iliyopita na tulikaa kwenye mahusiano kwa miaka miwili lakini kwa sasa hatupo wote”.

Abdu Kiba amekiri kuwa penzi lao lilikuwa la siri kutokana na mazingira waliokuwa nayo ambapo amesema sehemu yao kuu ya kukutana ilikuwa kwenye gari hivyo watu wao wa karibu sana ndio walioshtukia mchongo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.