Ali Kiba Aweka Wazi Wasanii Anaotaka Kuwasaini Rockstar 4000

Msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ambaye amesainiwa chini ya label ya Rockstar 4000 amefunguka kuwa wana mpango wa kuendelea kusaini wasanii wengi wenye vipaji chini ya label.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5, Ali Kiba alikiri kuwa hawezi kutangaza hadharani rasmi  kwa sasa kwani bado hawajakamilisha kila kitu lakini baadhi ya wasanii ambao wana mpango nao au aliowagusia ni pamoja na Aslay, Abdu Kiba , Abby skill na Jokate.

download latest music    

“Ni ngumu kuwataja kwa saivi kwasababu hatujawa introduce lakini Abdu Kiba yupo na Abby skills pia bila shaka nina uhakika naye atakuwepo”.

Ali Kiba alipouliza kuhusiana na Aslay kama wana mpango wakumchukua kutokana na kipaji chake, Ali Kiba amekiri kumkubali sana Aslay.

“Aslay ni msanii mzuri sana na anafanya kazi yake vizuri sana na anapendwa na watu na anaimba vizuri na ana talent na ni kweli Rockstar inachukuaga wasanii wenye vipaji kama Aslay lakini hatuja Fanya mazungumzo na Aslay bado lakini tunavyosema bado maana yake kuna nia huko mbeleni”.

Lakini pia Ali Kiba aliongelea kumsaini Mwana Dada Jokate ambaye pia alikuwa mpenzi wake na alifunguka:

“Jokate bado hajasaini lakini huwa anapendelea kuimba lakini ni mtu wa karibu wa rockstar anapendaga kutupa ushauri saa nyingine lakini pia ana talent ya kuimba na pia mda wowote akiwa tayari bila shaka tutamsaini”.

 

Ali Kiba ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Seduce me’ alioutoa mwezi uliopita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.