Alichokisema Nahrel Kuhusu Rosa Ree na lebel ya Afrika ya kusini

Mtayarishaji wa muziki kutoka katika kundi la Navy Kenzo nahrel amezungumzia msanii aliyewahi kumsaini katika lebel yake na kisa kuondoka na kuanza kufanya kazi zake mwenyewe Rosa Ree ambae kwa sasa anafanya vizuri sana ktika game kama rapper wa kike.

Nahrel amethibitisha kuwa msnaii huyo kwa sasa amepata dili nono la kusainiwa na moja ya lebel kubwa nchi afrika ya kusini inayojulikana  kama DIMO PRODUCTION ya nchini humo.

download latest music    

mimi nadhani tulichokifanya tumekifanya kwa uwezo wetu,tuliweza kutengeneza kitu ambacho kilionekana.we are proud kutengeneza wasanii kama yeye ambao leo hii wanaweza kuonekana kusainiwa na lebel nyingine ni dili kubwa sana na hata sisi tulivyoamua kuwasaini ilikuwa ni kwa ajili ya kuwasapoti.kwaio Rosa Ree anapopata dili lingine na mimi napata moyo wa kuendelea kusapoti wengine.ninaamini kuwa itamfikisha sehemu nyingine ambayo pengine mimi nisingeweza.

Rosa Ree alianza kufanya kazi na kundi hilo akiwa kama msani aliyesainiwa hapo na kutengenezwa katika kundi hilo mpaka pale iliposemekana kuwa kulitokea mtafarauku uliowafanya kushindwa kufanya kazi pamoja , lakini sasa hivi mambo yanaenda vizuri na kupata menejementi nyingine.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.