Aliyekuwa Dancer wa Alikiba, Msami,na Matonya Afariki Dunia.

Imethibitika aliyewahi kuwa dancer katika video mbalimbali za wasanii Tanzania Emma amefariki Dunia siku ya jana baaada ya kuugua kwa muda mrefu  kutokana na matatizo ya kifua.

Mcheza shoo huyo ambae alishawahi kutangazwa katika kipindi cha Shilawadu kipindi cha nyuma na kufunguka kuwaomba msaada wasanii mbalimbali ambao aliwahi kufanya nao kazi hatimaye amefutwa na mauti baada ya kuugua kwa  muda mrefu.

download latest music    

Emma alishawahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali akiwemo matonya katika wimbo wa zilipendwa akiwa kama kiongozi wa wachezahi wengie.alipowahi kuelezea matatizo yake, Emaa anasema kuwa kutokana na kipato kidogo walichokuwa wakikipata katika kufanya dancing iliwalazimu kufanya kazi nyingine tofauti na hiyo hivyo yeye alikuwa akiuza mitumba na kilichomsababishia kifua ni uzito wa begi la nguo alilokuwa akilibeba.

Akithibitisha kifo chake baba mzazi wa marehemu amewashukuru msanii kama alikiba, timbulo na matonywa kwa kipindi walichokuwa wakitoa misaada yao lakini pia ameomba kusaidia ili kumfikisha katika nyumba yake ya milele.

Katika ukurasa wake wa instagram, msamii alionyesha kufikiwa na taarifa hizo kwa kuweka baadhi ya picha za sms aliwahi kuchart na kijana huyo akiomba msaada.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.