Aslay Afunguka Kuhusiana na Ndoa Ya Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Aslay amefunguka na kuongelea ndoa ya staa wa Bongo wa fleva Ali Kiba iliyofungwa wiki iliyopita ambapo amesema haoni tatizo kwa Msanii huyo kuoa nje ya nchi.

Ali Kiba amemuoa mwanamke anayeitwa Amina Rikesh mwenye asili ya Kiarabu kutoka Oman lakini anayeishi Mombasa nchini Kenya.

download latest music    

Mashabiki walimtolea povu Ali Kiba kwa kitendo chake cha kuamua kwenda kuoa nje ya nchi wakati Tanzania kuna wanawake kibao jambo ambalo Ali kiba alijibu kuwa macho na moyo havina pazia.

Aslay ameipongeza na kusema watu wasishangae au kulalamika mtu kuamua kuoa nje ya nchi kwani jambo hilo ni la kawaida tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aslay amewataka mashabiki zake wasilalamike kitendo cha yeye kwenda kuoa nje ya nchi kwani ni jambo la kawaida sana kutokea:

Kuoa ni jambo la kheri bwana na ni hatua kubwa sana nampongeza sana kaka mkubwa kwani sio jambo la mchezo hilo, lakini watu wanatakiwa kuelewa kuoa nje ya Tanzania ni jambo la kawaida tu kama mtu anavyotoka kwenye kabila lake na kuoa kabila lingine“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.