Aslay na Nandy Kuburuzwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Wizi

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri kwa hivi sasa Aslay pamoja na msanii wa kike mwenye sauti ya kipekee kutoka THT, Nandy wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kutishiwa kuburuzwa mahakamani baada ya Luik a wimbo bila ruhusa.

Aslay na Nandy wanatamba hivi sasa na wimbo wao unaoitwa ‘Subalkheri Mpenzi’ ambao wanashika chati katika stesheni mbali mbali za redio na hata kukaa katika nafasi za mwanzoni katika mtandao wa nyimbo na video YouTube ambalo walishika nafasi ya kwanza kwa muda wa wiki nzima.

download latest music    

Kwenye ziara na vyombo vya habari waliyofanya   (media tour) katika jitihada za kutangaza nyimbo hiyo Aslay na Nandy waliwahakikishia mashabiki zao kuwa wamepata ruhusa kamili ya kurudiana kuuimba wimbo huo ambao ulishawahi kuimbwa siku za nyuma.

Sintofahamu imekuja kuzuka baada ya  mmiliki wa wimbo hu, kikundi cha Taarab asilia Visiwani Zanzibar (Culture Music club) kudai pesa zilizotolewa jumla ya shilingi 800,000 kama fidia ya wao kutumia kazi yao hawazitambui hivyo wanajipanga kuwapeleka mbele ya mahakama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Katibu mtendaji wa kikundi hiko Taimur Rakuni amedai kuwa wasanii hao kabla ya kuimba wimbo huo upya walitakiwa kuonana na uongozi huo ili kukubaliana jambo ambalo hawakufanya hivyo.

Kwa msanii Aslay hii ni mara ya kwanza kwake anakumbana na skendo hii ya kuiba wimbo wa wasanii wengine lakini kwa Nandy ametuhumiwa mara nyingi na wasanii wengine kwa kuiba nyimbo na kuzirudia bila ruhusa mfano ni Ray C ambaye alimjia juu na kudai kaiba wimbo wake na kuuimba bila ruhusa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.