Aunty Lulu Asherekea Mama Yake Kupata Mchumba

Msabii wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu Kama Aunty Lulu amefunguka na kutangaza furaha yake Baada ya mama yake mzazi kupata mchumba na hatimaye kuchumbiwa.

Aunty Lulu amesherehekeamama yake mzazi kupata mchumba ambaye alimvalisha pete mwishoni mwa wiki iliyopita katika kanisani moja lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Aunty Lulu alisema kuwa amefurahi sana mama yake kumpata mwenza kwani baada ya baba yake kufariki dunia, alikaa muda mrefu akiwa mpweke.

Unajua nina furaha kupita kiasi mama yangu kupata mwenza imenipa faraja, ninamuombea maisha mema ya ndoa kwani ni jambo ambalo limetufurahisha sisi kama familia”.

Aunty Lulu ameweka wazi kuwa mama yake hakuwa kwenye mahusiano na baba yake kwa miaka mingi hivyo vyema mama yake kuuaga upweke na kupata furaha.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.