“Babu Tale Alinitambulisha Kwa Ruge”- Zamaradi

Mtayarishaji na Mdau wa filamu za Bongo movie Zamaradi Mketema amefunguka na kuongelea mahusiano yake na baba Watoto Wake Ruge Mutahaba.

Kwa miezi kadhaa sasa Ruge amekuwa hospitali nchini Africa ya Kusini ambapo ndugu zake wamejitokeza na kuomba msaada kwa Watanzania kutokana na matibabu kuwa makubwa kupitiliza.

download latest music    

Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wamekuwa waliwaalika wadau mbalimbali ambao wanaguswa na maisha ya Ruge na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu mwanaharakati huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

Siku ya jana alialikwa Zamaradi  ambaye ni mama watoto wa Ruge ambapo amefunguka mambo mbalimbali pamoja na namna alivyokutana na bosi Ruge.

Tulikutana na Ruge kwenye mazingira ya kazi, na mimi nimemjua Ruge kupitia Babu Tale. Tale ndio mtu ambaye alinitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza, alinipa namba yake akanimbia mtafute huyu bwana lakini usimwambie kama mimi ndiye niliyekupa namba”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.