Babu Tale Ametoa Sababu Iliyopelekea Diamond Kuzomewa Kwenye Tuzo

Meneja wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuelezea sababu iliyopelekea mpaka Diamond kuzomewa kwenye tuzo.

Mwishoni mwa mwaka 2017 Diamond Platnumz alichaguliwa kushiriki tuzo za Soundcity Music Awards ambapo alikuwa anashindana kwenye kipengele cha The best Male MVP of the year 2017 ambayo alishinda na kuwabwaga wasanii wakubwa wa Nigeria kama Davido na Wizkid pamoja na wengineo.

download latest music    

Lakini cha ajabu baada ya Diamond kutangazwa mshindi watu waliokuwa ukumbini hapo waliishia kumzomea vibaya mno na jambo lililoashiria kuwa hawakufurahishwa na  ushindi huo lakibi pia Wanigeria walipiga sana vita ushindi huo wa Diamond mtandaoni.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online Babu Tale ameeleza sababu kubwa zilizopelekea Diamond kuzomewa:

Unajua zile ni tuzo za Nigeria na walikuwa sio tu wanazomea bali walikuwa wanamzungumzia mtu wao ambaye walitaka ashinde lakini aliyefanya vizuri ni Diamond kwa sababu mashabiki zake walimpigia kura name unajua kwanini Wanigeria wao walipiga kelele? Kwanza wenyewe wako wengi Alafu wanakuwa wanajiona wao kama ndio wanaendesha mziki Wa Africa alafu huyu anatokea Tanzania sehemu ambayo ina watu wachache Lakini mwisho wa siku ni wivu kwao kuona kwanini tuzo haikai kwao imeondoka imekuja kwetu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.