Baraka the Prince:Nisingekuwa Msanii Ningekuwa Mwanajeshi.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Baraka the Prince amefunguka na kusema kuwa endapo hasingekuwa katika tasnia ya muziki basi angekuwa anafanya kazi ya uanajeshi kwa sababu anaona kabisa kuwa ni kazi anayoendana nayo na anahimili kuifanya.

Baraka ambae alikuwa akifanya mahojiano na kipindi cha Eight cha TVE, anasema kuwa anapenda kazi ya uanajeshi na kusema vitu vitano ambavyo vinamvutia sana kwa wanajeshi.

download latest music    

napenda sana mazoezi ya wanajeshi, napenda na ule mchaka mchaka  wao, lakini pia napenda hata mavazi yao , napenda attitude yao   na pia ni wakarimu sana nawapenda hapo lakini pia  napenda the way walivyo.

Baraka the Prince ambae kwa sasa anatamba na kibao cha sometimes anafanya kazi chini ya lebo yake mpya aliyotengeneza mwenyewe inayojulikana kama Bana Music baada ya kutoka katika uongozi wa Rockstar4000  ambapo walikuwa wakifanya kazi pamoja na Alikiba na ndipo alipo Ommy Dimpoz kwa sasa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.