Barnaba:Nahitaji Wasanii Wa Kike Sana

December 15, 2017 at 09:56
Barnaba:Nahitaji Wasanii Wa Kike Sana

Msanii wa muziki wa bongo fleva Barnaba Elias maarufu kama Barnaba classic ambae kwa sasa ana lebel yake na anafanya production ya muziki amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ataanza kusadia wasanii wengine wachanga lakini anahitaji wasanii wa kike sana kuliko wa kiume katika kufanya nao kazi.Barnaba ambae ataanza kufanya kazi na wasanii wachanga ifikapo mwakani anategemea kuanza na wasani wa kike watatu kwanza ili kuangalia upepo unavyokwenda pia.

Mimi lebel yangu ni changa na hata mwaka jana nilisema kabisa kuwa  nitawatambulisha na kuwatoa wasanii mwakani nikianza na mula, na baada ya hapo nitaanza kuchukua na chapa nyingine , in fact nimesema ninahitaji wasanii wa kike sana ninahitaji wa kike watatu. –Alifunguka Barnaba

Barnaba alipoulizwa sababu ya kuchagua wasanii wa kike tu na sio wanaume alisema kuwa wasanii wengi wa kike hawapati nafasi ya kuingia katika game na ukiangalia katika industry ya muziki wasichana ni wachache kuliko wanaume.Hivyo anataka kuibua wanawake pia, lakini pia Barnaba anaamini kuwa kwa sababu yeye pia ni mtunzi na nyimbo zake nyingi zinahusu mapenzi na ziznendana sana na wasichana basi hii itakuwa ni nafasi nzuri kufanya kazi na watu hao.

Loading...

kwaiyo kwa upande wa kiume atabaki mula peke yake, na sababu yangu ni ya msingi sana kwa sababu wanaume tupo wengi sana ktiak game,na kitu kingin mimi pia ni mwandishi na nyimbo zangu nyingi huwa zinzendana na wasichana  na nimeamua kuwa hivyo na am sure mtu kama Diamond alishasaidia sana.- Alimalizia Barnaba.

Akiwa kama mtu aliesaidiwa mpaka kufikia hatua yakusimama na kufikia level aliyofikia barnaba hana budi kusaidia wengienwalopo mtaani ambao pia wana kipaji cha kufanya vizuri kama yeye.

Barnaba ni moja ya wasanii wakubwa wanoweza kutajwa katika list ya wasanii walioanza toka chini kabisa na kuweza kufika pazuri sana alipofika leo, ni mwalimu wa muziki kwa watu wengine lakini pia amekuwa mwandishi mzuri wa nyimbo zake na za watu wengine pia.

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.