BASATA Wahaidi Kumshughulikia Sanchi

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limehaidi kumshughulikia Socialite maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Janey Rimoy maarufu kama Sanchi kutokana na picha zake zenye utata.

BASATA wametoa tamko hilo baada ya kupokea malalamiko kwa Watu wengi za kwanini Mrembo huyo amekuwa akiposti picha za nusu uyupu lakini amekuwa akiangaliwa tu.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Afisa Habari wa BASATA, Agnes Kimwande alisema kwanza hawamtambui Sanchi kama mwanamitindo na hawajui ni kazi gani maalum ambayo anaifanya ndiyo maana walisita kumchukulia hatua ila watafuatilia kama ni kweli anajihusisha na kazi za sanaa ili wamchukulie hatua mara moja na sio kwamba wanamuogopa.

Watu wengi wanatumia kivuli cha sanaa kufanya mambo ambayo kimsingi sio mazuri sio kwamba tunamuogopa kumchukulia hatua, hapana ila sisi hatumtambui huyo Sanchi kama ‘Model’, kwa sababu sisi tunamchukulia hatua mtu ambaye anafanya makosa kwenye kazi ya sanaa mfano Diamond akivua nguo akiwa anafanya shoo tutamshughulikia kwa sababu inatuhusu sisi moja kwa moja ila naahidi tutamfuatilia kama kweli anafanya sanaa ili tujiridhishe kama anatuhusu basi tutamshughulikia“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.