Ben Pol Anamtamani Sana Papii Kocha.

Msanii wa muziki nchini Ben Pol ambae kwa sasa anafanya vizuri katika soko la muziki nchini amefunguka na kusema kuwa  kiu yake kubwa sasa hivi ni kufanya  kazi na Papii Kocha na akipatiwa nafasi hyi hawezi kuichezea kwa sababu anamuna ni msanii anayeweza sana kimuziki.

Ben Pol ansema kama endapo atapata bahati ya kufanya kazi na papii kocha hatokaa aichezee nafasi hiyo kwa sababu ni mtu mwenye kipaji na ataacha kila kitu alichokuwa anakifanya na kwenda kufanya nae kazi.

download latest music    

kitokea nimepata nafasi ya kufanya kazi na papii kocha yaani hapo hapo naacha kila kitu nilichokuwa nakifanya naenda  kukesha studio kuhakikisha  nafanya kitu bora, kwa sababu papii ni mtu mwenye kipaji cha kipekee sana

Papii Kocha ambae hivi sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya cha waambie amepokelewa vizuri na mashabiki wake baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika muziki kwa sababu ya kutumikia kifungo cha muda mrefu walichohukumiwa kwa kosa la kulawiti yeye na baba yake.

Hata hivyo wawili hao walipata msahama wa Raisi na kurudi uraiani ambapo serikali pia imejitahidi kuingiza mkono wao ili kuweza kuwasaidia kuinuka kimuziki.

Ben pol ambae sasa hivi amekuja na muonekano mpya wa kuweka nywele rangi ya kijanii amekuwa akifanya vizuri na kukubalika sana katika list ya wasanii wa bongo walikuja na kuweka mapinduzi makubwa ya muziki na kuwateka mashabiki zake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.