Black Rhino Kurudi Kwenye Muziki Baada Ya Kimya Kirefu

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Nicholaus Haule ‘Black Rhino’ ambaye pia ni mdogo wa legend wa Bongo fleva Joseph Haule ‘Profesa jay’ ametangaza kurudi kwenye gemu la Bongo fleva baada ya kimya cha miaka mingi.

Black Rhino alifanya vizuri sana miaka ya nyuma lakini alikuwa kimya kwa miaka zaidi ya mitatu bila kuachia ngoma yoyote lakini ameamua kurudi rasmi na kuachia wimbo wake unaoitwa ‘Panda mnazi” ukiwa na maaana ya kulegeza vyuma.

download latest music    

Kwenye Interview aliyofanya na Showbiz, Black Rhino amesema ujio wake huo unamaana kubwa hasa kwa vijana wa sasa kwani unafanya kila anayesikiliza kusahau shida:

Yaani Panda Mnazi ni sawa na kusema kula shangwe, ni ngoma f’lan hivi ya weekend, ya klabu ambayo ikipigwa lazima upagawe.

Nimekuja kitofauti kwani ngoma ipo katika mahadhi kama ya ile ngoma ya mistari ambapo kuna mchanganyiko wa Hip Hop na Raga”.

Ngoma ya Mnazi imetengenezwa na Mr. T Touch huku ‘video’ yake ikikisimamiwa na Kwetu Studios.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.