Bob Junior- Acheni Kuingilia Kati Bifu Langu na Diamond

Aliyekuwa Producer wa Diamond Platnumz ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva Bob Junior, Amewataka mashabiki kuliacha kama lilivyo swala lake yeye name Diamond kwani hakuna anayejua mwanzo wa kazi zao.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya mpya ya ‘Give me’ ameiambia Bongo dot home ya Times FM kuwa mashabiki wanaingilia Kati kitu wasichokijua kiundani kitu ambacho sio sawa.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya Bob Junior alisema;

“Ukweli ni kwamba hawapaswi kunizungumzia na yeye kwasababu kipindi tulikuwa tunatengenezana tulikuwa wawili, kwa hiyo huwezi kuingilia wewe kama shabiki maandazi kea kuingilia vitu ambavyo huvijui. Mimi na yeye  tulikuwa tunafahamiana wakati tupo chumbani, wakati chumba ni studio lakini baada ya hapo tukawa wakubwa, sasa wewe shabiki ambaye unazungumza unamjua yeye? Au unanijua Mimi? Au Mimi na  yeye ndo tunajuana vizuri name zaidi”.

Pia ameongeza Kuwa;

“Kwa iyo wewe unaingia Kati baada ya kumfahamu Bob Junior na huyo muhusika (Diamond), unanza kumtetea yeye au kunitukana mimi wakati sisi hutuwafahamu?”.

Bob Junior amekuwa akimshutumu Diamond kwa kutangaza Kuwa kuna kolabo ambayo wangefanya pamoja lakini hakuna utekelezaji wowote na amekuwa akimtafuta ili kuzungumza hilo lakini Diamond amekuwa akimpuuza.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.