Bodi Ya Filamu Yamfungulia Wema Sepetu

Bodi ya filamu Tanzania siku ya leo imetangaza kumfungulia Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu Baada ya kumkingia kwa miezi kadhaa na kujihusisha na Shughuli zozote za kisanaa.

Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB),  Joyce Fissoo, amesema  Wema amefuata maelekezo aliyopewa na bodi hiyo kwa asilimia 75.

download latest music    

Hatujamfungulia sababu ya huruma, tumemfungulia sababu amefanya tuliyoagiza kwa zaidi ya asilimia 75“.

Mwaka jana mwezi wa kumi Bodi ya filamu ilitangaza kumfungia Wema na kujihusisha na Shughuli zozote za kisanaa Baada ya Msanii huyo kusambaza picha zake za utupu katika Mitandao ya kijamii.

Kabla ya kufungiwa, Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambalo lilimuonyesha akiwa faragha na mwanamme anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.