Chaz Baba Adaiwa Kubadili Dini Ili Aoe Mke Mwingine

Msanii wa muziki wa Dansi nchini kutokea bendi ya The African Stars band ‘Twanga Pepeta’ Charles Gabriel maarufu kama Chaz Baba amedaiwa kuabadilisha dini ili apate kuoa mke mwingine.

Global Publishers wanaripoti kuwa Chaz Baba anadaiwa kubadilisha dini kutoka Ukristo kwenda Uislam ili aweze kuoa mke mwingine huku ndoa yake ya kwanza na mwanamama Rehema Sospeter ambaye alifunga naye kanisani ikidaiwa kuvunjika.

download latest music    

Inaripotiwa kuwa kulikuwa na mgogoro wa mda mrefu kati ya Chaz Baba na mkewe huyo kiasi ambacho kuna kipindi mkewe huyo alikuwa akiondoka na kurudi kwao kisha kurejea tena kwa mumewe. Ilisemekana kwamba ilikuwa ni kawaida yao kutofautiana na kuyamaliza, lakini safari mkewe aliondoka na hakurudi tena.

Baada ya mkewe kugoma kurudi ndipo Chalz Baba alianza harakati za kutaka kuoa Mke mwingine kwa kubadilisha dini.

Baada ya Tetesi hizo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Chalz Baba ili kupata ukweli wake ambapo alikiri kubadilisha dini na kusisitiza anaoa mwanamke ambaye sio maarufu baada ya Tetesi kuwa anataka kumuoa muigizaji wa Bongo movie Husna Sajent.

Ni kweli kabisa na sasa hivi ninaitwa Adulkarim na ndoa yangu ni mwezi ujao (mwezi wa kumi na moja).

Sajenti? (kicheko) hapana, mke wangu mtarajiwa siyo maarufu hata kidogo. Yeye yupo bize na kazi zake tu maana ni mfanyabiashara“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.