Chemical Akubali Kushushwa na Singeli.

Baada ya mashabiki kumtupia maneno na kumwambia kuwa amekaa kipindi kirefu bila kutoa nyimbo mpya hivyo kusemekana kuwa amefulia aliamua kuja na kujinadi kuwa hata siku moja yeye hawezi kufulia kwa sababu kwake ni kama kiwanda cha muziki kila siku zinatengenezwa nyimbo mpya.

Msanii wa kike wa Rapper Claudia Lubao maarufu kama Chemical amesema kuwa tangu ameanza kuimba singeli ndipo ameanza kuona kama muziki wake umeshuka kwa sababu muziki aliokuwa akiufanya ulikuwa ni mkubwa sana.

download latest music    

Chemical anasema kuwa heshima yake kwa mashabiki imeanza kushuka tangu alipoanza kujiingiza katika singeli kwa sababu kupitia muziki wake wa kuchana alikuwa tayari ameshawaaminisha mashabiki kuwa anaweza kukaa kwenye game.Hata hivyo Chemical anasema kuwa ingawa singeli inamleta mashabiki wapya ambao ni wapenzi wa singeli lakini wale waliokuwa wakipenda muziki wake wa kuchana wamemshusha thamani ana na wengine atakuwa amewapoteza.

Ukweli ni kwamba siamini sana kupitia muziki wa singeli,ninaamini kuwa muziki niliokuwa naufanya hapo awali ulikuwa mkubwa sana kuliko hata huu wa singeli wa sasa.-Alifunguka Chemical.

Kwa kuongea kuhusu muziki huo wa singeli na hisia za mashabiki wake , Chemical anasema kuwa kwa sasa hajafikiria kabisa kuufanya tena muziki huo labda baadae sana kwa sasa anataka kurudi kwa mwanzo ili kuwaridhisha mashabiki wake wa mwanzo.

Mwaka uliopita Chemical aliamua kufanya singeli ya wimbo uliojulikana kwa jina la kama ipo ipo tu ambao sasa hivi anakiri kuwa uamuzi wake huo umefanya hshima ya muziki wake ishuke na kupoteza baadhi ya mashabiki.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.