Chid Benz Aitabiria Makubwa Bongo Fleva Ya Sasa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Dar Es Salaam Stand Up’ amefunguka na kudai anaona kuwa Bongo fleva ya sasa inazidi kufika mbali tofauti na zamani.

Chidi Benz amedai kuwa kwa jinsi anavyoona sasa wasanii wa Bongo fleva wamekuwa wanajituma sana tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma kwa wasanii wengi.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers Chid Benz amesema kuwa, muziki wa Bongo Fleva una­piga hatua siku hadi siku kutokana na wasanii wanavyojituma, hivyo utafika mbali zaidi.

Muziki wa Bongo Fleva un­aweza kufika mbali zaidi kwa kuwa wasanii wanaonekana kujituma zaidi, kila siku ki­nakuja kitu kipya, wanaonye­sha uwezo mzuri wa kuhitaji kufika mbali“.

Kadri miaka inavyozidi Kisonga mbele ndivyo sanaa ya Bongo fleva imezidi kupiga hatua na Kusonga mbele zaidi kutokana na wasanii kupata changamoto kutoka kwa wasanii wengine.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.