Chid Benz: T.I.D Ananiita Mimi Teja Mwambieni Aache Unafki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Chid benz na  msanii mwenzie T.I.D wameingia katika bifu zito baada ya kauli aliyoitoa  T.I.D alipoulizwa kuhusu Chid benz kwenye mahojiano  aliyoyafanya.

Chid Benz amekuwa katika skendo ya kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu ambapo mapema mwaka huu alipelekwa ‘rehab’ na Babu Tale lakini baada ya muda mfupi aliondoka na kusema kwamba ameacha kutumia madawa ya kulevya na kurudi kwenye muziki lakini baada ya muda mfupi ilisemekana amerudia tena kutumia madawa. Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni T.I.D aliulizwa anashauri ni vipi Chid Benz asaidiwe ili aache kutumia madawa ya kulevya T.I.D alijibu:

download latest music    

“Ukiniuliza mimi kabisa kabisa kutoka katika moyo wangu kabisa apelekwe detention thats the best we can do kwa sababu mkimuacha nje atarudia kufanya yaleyale, mpeleke detention piga pingu akitulia ndo mnamtoa pingu mpaka akili yake ikae sawa ndo mnamwambia akafanye mziki wake, Mimi sina urafiki na Chid mimi sio kaka yake, baba yake wala ndugu yake kwaiyo sijali wala nini”.

Chid Benz ambaye aliumizwa na maneno hayo aliyoyasema T.I.D aliyedai ni rafiki yake alimwaga povu hili:

“Kama T.I.D amesema  mimi sio mtu wake wa karibu kwa hilo mi naweza kumwambia ni mnafki mkubwa sana kwasababu kila mtu anajua ni mtu wangu wa karibu sana yaani mshkaji wangu sana nilishawahi kumuachia mpaka gari yangu atumie ilikuwa starlet ya kawaida mi nikawa natumia BMW alikuwa mtu ambaye hana gari nikamwambia we huna gari tumia hiyo starlet na alishakuja kwangu mara kadhaa akalala kwangu so ni mtu wangu wa karibu so kama kasema hivyo alikuwa kachanganyikiwa  au keshapata vitu vingine kichwani vimemfanya aongee uongo “.

Wasanii hao wote wawili wapo kwenye skendo za kutumia madawa ya kulevya lakini wakiulizwa kila mmoja hukataa na kumnyoshea kidole mwenzie. T.I.D alikamatwa mapema mwaka huu na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia na kuuza madawa ya kulevya baadae alikiri na kuhaidi kuacha lakini bado watu wanamshuku kuwa kutokana na tabia zake hajaacha kutumia madawa ya kulevya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.