Loading...

Dhamana Ya Amber Rutty Yaibua Mazito

December 06, 2018 at 10:40
Dhamana Ya Amber Rutty Yaibua Mazito
Loading...

Wiki chache zilizopita Msanii Amber Rutty na Mpenzi Wake Said Mtopali waliwekwa ndani kufuatia kesi yao ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Amber Rutty alifanikiwa kupata dhamana Novemba 27, mwaka huu na kuonekana ameambatana na Mchungaji Daudi Mashimo mahakamani hapo, watu wengi waliamini kwamba mchungaji huyo ndiye aliyemuwekea dhamana.

Loading...

Lakini Baada ya Gazeti la Amani kuzungumza na mama yake mkubwa Amber Rutty aitwaye Asha Seif ambaye alisema mbali na watu kuamini hivyo, alimshangaa Mchungaji Mashimo kuendelea kuwaamisha watu hivyo wakati si kweli.

Mimi nashangaa, huyu mchungaji alikuja siku ile pale mahakamani akakuta mimi pamoja na wifi yangu tumeshakamilisha taratibu za dhamana, akaja huyo Mashimo, akaniambia anaomba anisaidie kumtoa nje Amber Rutty maana kuna fujo ya waandishi wa habari.

Kwa kuwa mimi nilikuwa sijui sana mambo ya mahakamani, nikamkubalia kweli akafanya hivyo. Sasa baada ya kunisaidia, nikashangaa mara ooh sijui anampeleka kanisani, sijui mara atambadilisha dini, kwa kweli amenisikitisha sana”.

Mchungaji Mashimo mchungaji huyo ameeleza ukweli wake kuwa yeye alimuwekea dhamana jamaa wake Amber Rutty, Said MtopalI na  sio Amber Rutty:

Mimi nilimuwekea dhamana Mtopali japo nilikuwa na lengo la kuwawekea wote wawili lakini bahati nzuri mama yake amemuwekea dhamana Amber Rutty basi mimi nikamuwekea Mtopali”.

Lakini pia Mchungaji Mashimo aifunguka kuhusu suala la kujitangaza kumbadili dini Amber Rutty ambapo alisema ishu hiyo haina ukweli wowote kwani yeye alimkaribisha kwenye maombi na si kumbadili dini.

Share

Comments

  1. Daaaaaah

  2. Huyu pastor hatari kiukweli

  3. Sijaona mchungaji anapenda fame kama huyu kiukweli

  4. Huyu anakula kiki anaoga kiki

  5. ??? anaudhi kweli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…