Diamond Akiri Kuwa Yeye ni Bingwa Wa Kiki na Drama

Supastaa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekiri kuwa yeye ni bingwa wa kutafuta kiki mitandaoni Lakini pia anajulikana kwa kuwa na drama zisizoisha.

Diamond amekiri hayo kwenye mkutano aliofanya na waandishi habari siku ya jana katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kujuzwa mambo kadhaa kuhusu sheria za mitandao.

download latest music    

Diamond ameongea hayo na kuomba radhi kwa mashabiki zake na serikali baada ya kuachia video mbili tofauti zilizomuonyesha akiwa na wanawake wawili huku akifanya matendo yaliyotafsiriwa kinyume na maadili ya Kitanzania.

Na mimi ni miongoni mwa mabingwa wa kiki, najikubali, najua kabisa drama ninazo kila siku lakini tunaziweka vipi zisiende kuwatia dosari viongozi ambao wanapambana kuhakikisha sanaa yetu inafika mbali,

Kwa sababu ikienda kwa mazingira ambayo yalikuwa yamezoeleka huko nyuma unawavunja moyo viongozi ambao wanapigania sanaa ifike mbali”.

Lakini pia kwenye mkutano huo pia Nandy aliomba radhi pia kwa kusambaza video yake ya chumbani na Billnas ambayo ilivuja wiki chache zilizopita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.