Dudu Baya amsifia Chidi Benz

Msanii mkongwe katika  style ya ku-rap nchini Tanzania  tangu miaka ya 90’s mpaka sasa  na msanii ambaye ukitaja  wasanii wakubwa wakongwe  waliosaidia kukuza na kuinua muziki wa Tanzania basi huwezi kumuacha msanii huyu, si mwingine ni Dudu baya,Dudu baya ni msanii wa Bongo Fleva  ambae amepitia mengi  mpaka kufikia hapa alipo katika muziki.

Akiongea katika interview aliyoifanya hivi karibuni kupitia kipindi cha eNews cha EATV Dudu baya ameonekana kumsifia msanii mwenzie ambae pia ni mkongwe katika fani hii ya muziki Chid Benz,pamoja na kwamba katika kumbukumbu inaonyesha kuwa Dudu baya ni moja kati ya wasanii ambao waliongea vibaya kuhusu maisha ya msanii Chid Benz hapo awali na kumponda huku wakisema kuwa hawezi kubadilika tabia yake ya kutumia madawa ya kulevya na wala hatoweza kusikiliza watu wanachomwambia. lakini leo ameamua kubadilika na kumsifia Chid Benz, na anaamini kuwa Chid amebadilika .

download latest music    

“Nampa big up, amerecover ,namsifia sana ,sina doubt na yeye na namkubali sana “,  pia alimpa ushauri Chid “ni kama mdogo wangu, mimi ni kaka yake, sitaki arudi tena kwenye madawa ya kulevya,Mungu amuinue,Mungu amsamehe,na Roho Mtakatifu amsaidie  “aliongeza Dudu baya huku akimuombea pia.

Alipoulizwa kwanini mara ya kwanza alikuwa akimponda na sasa hivi anaonekena kumsifia ,Dudu baya alijibu” baada ya kuona anaelekea ninapopata…na tulishakutana mara mbili namuona yuko fresh.. kwenye mic namkubali, ana pumzi…hakuna Dar Es Salaam bila KingKong’ aliongezea Dudu baya.

Hata hivyo Dudu baya alisema kuwa “Mungu alisema tuombeane, mimi ninamuombea,shetani yule aliyemkamata kipindi kile asimrudie tena”

Chid Benz pia ni msanii mkongwe wa Bongo Fleva ambae alikumbwa na kashfa ya utumiaji wa madawa ya kulevya, ambapo matumizi hayo yalimpelekea kushuka kimuziki na kupotea katika ramani ya sanaa, lakini kwa sasa Chid amerudi tena huku bado akisuasua kidogo, hivyo Dudu Baya kama msanii mkongwe pia aliamua kumuongelea msanii mwenzie na kumpa moyo ili aendelee kufanya vizuri katika kazi zake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.