Dudu Baya Amwagia Povu Kali Mwanaye Wille Baada ya Tuhuma za Kumtelekeza

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Dudu Baya ambaye kwa muda sasa amekuwa akishutumiwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kumtelekeza mtoto wake wa kiume mwenye miaka 17 anayeitwa wille ambapo inasemekana kuwa Dudu Baya alikataa kumsomesha mtoto huyo.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Bongo 5 Dudu Baya alikataa tuhuma hizo na kudai kuwa alimlea mwanaye huyo kwa miaka kumi na tatu hivyo hawezi kumtelekeza;

download latest music    

“Mara ya mwisho nilimtafuta Wille akaja Mikocheni tukalala mpaka kesho yake nikampa zawadi zake zilikuwa pea mbili za raba tukaaga kuwa anarudi shule lakini hapo kuna tetesi nilisikia kuwa na yeye anaimba muziki anaimba maskani huko Mwananyamala kwaiyo kama mzazi nikajiuliza kama mzazi na mtoto wamekutana halafu humwambii baba ako kuwa unaimba na baba ako ni star, baadae napita mitaani naambiwa Wille anapatikana tu hapa maskani hayupo shule wala nini na shule ameshaacha Dah! kiukweli kama mzazi nilishtuka kwa sababu nampenda sana mwanangu na mi nimeishi tangu mdogo mwaka 2013 ndo mama yake alimuomba nikampa lakini nilikuwa naclear kila kitu lakini nimekuja kusikia ameacha shule kwa miezi tisa wakati nilikuwa nalipa ada kama kawaida na matumizi mengine lakini kinachonishangaza zaidi mama yake anajua haya yote lakini nasikia na mama yake yupo upande wake na wanagawana pesa za shule”.

Dudu Baya aliishia kwa kumwagia povu mwanaye;

“Lakini kwa kitendo alichofanya cha kuacha shule kuwa anakamatwa na polisi akalala ndani  Mimi kama Dudu Baya na baba yake sina kinyongo naye wala sina chuki naye japo amenidanganya anasoma shule kwa miezi tisa na haendi shule na anipiga hela kwa hilo nimemsamehe kwa kuwa ngamia huwezi ukampeleka kisimani ukamchapa anywe maji kama kaamua kuacha shule ni kijana wa miaka 17 siwezi kumlazimisha kwani anajitambua kama mi nilimwambia twende kulia kataka kwenda kushoto kila lakheri huko kushoto kwani maandiko matakatifu mwenyezi Mungu aliandika ‘mtoto mwenye hekima na busara humfurahisha babaye’ na toto jinga shenzi na pumbavu ni mzigo kwa mama na sio zigo kwa baba kwaiyo kwangu mimi simtafuti akiwa tayari anitafute aniombe msamaha kwani milango kwangu iko wazi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.