Dulla Makabila Kamuacha Husna Sajent na Kutembea na Rafiki Yake

Mkali wa muziki wa Singeli Abdallah Mohamed maarufu kama Dulla Makabila amedaiwa kufanya mazito kwani imedaiwa baada ya kumbwaga aliyekuwa mpenzi wake Husna Sajent hivi sasa anatembea na rafiki yake kipenzi Tiko.

Muigizai wa Bongo movie Husna Sajent na Dulla Makabila walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu hadi kuna muda walitangaza kufunga ndoa lakini baadae wakaachana baada ya familia ya Dulla kumkataa Husna.

download latest music    

Habari za kimbea zinadai hivi sasa Dulla Makabila amewachanganya vibaya mno waigizaji hawa wa Bongo movie ambao ni Husna Sajent na Tiko Hassan ambao walikuwa marafiki wakubwa lakini sasa inasemekana ni maadui wakubwa baada ya kuibiwa bwana.

Tiko

Baada ya habari hizi kusambaa gazeti la Ijumaa Wikienda lilimsaka Husna na kumuuliza kuhusu tuhuma hizo:

Ni kweli kabisa Dulla aliniacha na yuko na Tiko kwa hivi sasa lakini mimi nimeshaanza kusahau hayo mambo nipo na ninaendelea na maisha yangu kwa hivi sasa”.

Baada ya hapo gazeti hilo lilimtafuta Dulla Makabila ili kupata ukweli wake kuhusu ushindani hiyo na alifunguka:

Kwa hivi sasa niko na Tiko ndiye mpenzi wangu lakini kuna vitu vilinifanya nifanye hivyo kuhusu suala la kuwachanganya mimi nilianza kumjua Tiko kabla ya Husna ni mwanamke aliyekuwa akilini mwangu na hata hivyo sioni kama kuna shida hata kama walikuwa wanajua na ilimradi nimeshuacha mmoja nipo na mwingine”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.