Ebitoke Akumbwa Na Tuhuma za Kuiba Mume wa Mama Ashura

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini kutokea katika kundi la timamu Ebitoke  ametuhumiwa kuhusishwa na kuvunjika kwa ndoa ya msanii mwenzie Mama Ashura wa kundi hilohilo kwa kutembea na mume wake.Tuhuma hizo ziliibuka juzi kati mbaada ya mwana harakati Mange Kimambi kuamua kusema siri hiyo ambayo ilikuwa imejificha kwa  muda mrefu na kutoa hadi video zinazomuonyesha Mama Ashura akiwa barabarani na mtoto wake wa kiume wakiangaika baada ya kufukuzwa katika nyumba hiyo.

Ebitoke anaedaiwa kuwa alikuwa akikaa kwenye nyumba ya Mama Ashura na mume kwa muda kidogo ikiwa ni kama kumsaidia mahali pa kuishi aliamua kumgeuzia kibao shoga yake huyo na kutembea na mume wake ambae pia ndio meneja wa kazi zao za uchekeshaji.

download latest music    

Mpaka sasa inavyosemekana ni kwamba baada ya Mama Ashura kufukuzwa katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe, Ebitoke ndio amekuwa mama mwenye nyumba hiyo na kumuacha rafiki yake akiangaika na mtoto barabarani.

Tetesi hizo zinadai kuwa hata baada ya Mama Ashura kufukuzwa , hakuruhuiswa kuondoka na kitu chochote na kwamba hata akaunti zao za mitandao ya kijamii meneja wao huyo ndie anaezimiliki hivyo hawajui hata neno la siri la kuingilia katika akaunti zao.

Ni kawaida kwa wasanii bongo kupinduana na kuchukuliana mabwana  hata kama wawili hao wanakuwa ni marafii sana, na hii inafanya kuharibu kazi zao na mahusiano yao mazuri katika kazi yanakuwa yanaishia hapo .

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.