Ebitoke Atangaza Kujitoa Timamu Africa

Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii ameweka wazi kuwa ameachana Rasmi na Management ambayo ilikuwa inamsimamia Timamu Africa.

Ebitoke ametoa taarifa hizo Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka wazi sababu ya kuacha kufanya nao kazi ni kwa sababu ya mkataba wao kuisha muda wake.

download latest music    

Napenda kuchukua nafasi hii na kuwatarifu Mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, kuanzia sasa nitakua nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV, nikimaanisha mkataba wangu umeisha.

Wamekua wema na wenye UPENDO KWANGU SIKU ZOTE. Pia Napenda kuwashukuru Mashabiki zangu kwa kipindi chote ambapo mmekua mkinisapot na kufurahishamwa na kazi zangu ?”.

Lakini pia Ebitoke ametoa shukrani zake za dhati kwa management yake hiyo ambayo pia imesimamia comedians maarufu kama Mama Ashura na Mkali wao.

Shukukran ZANGU ZA Dhati kwa Manager wangu ?@timothconrad kwa kunilea vyema nitakupenda siku zote Maana bila wewe nisingekua mimi. @bwanamjeshi, @mr_beneficial, @chidi_luba nawashukuru sana kwa upendo mlionao kwangu tangu tumeanza kufanya kazi mpaka sasa, nyie ni familia yangu, tutaendelea kusapotiana kama familia ❤”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.