Eric Shigongo Asema Menejiment ya Daimond Ndio Sababu ya Kugombana Kwao

Mjasiramali na mtunzi wa vitabu kutoka nchini  Tanzania Eric shigongo amefunguka mazito kuhusu bifu lililokuwepo kati yake na msanii Diamond Platinumz na kusema kuwa sababu kubwa ya kutokupatana kwao ilikuwa ni uongozi wa Diamond ambao haukuwa unamuongoza kama alivyotakiwa kuongozwa.

Katika makala yake ndefu aliyoiandika, Eric alianza kwa kumpongeza lakini hku akisema kuwa alichokifanya mwaka huu ndicho kilichowagombanisha miaka kadhaa iliyopita na menejiment yake kwa sababu ya tamasha aliloliandaa ambalo lilikuwa la wazi kwa wananchi wa Tandale.

download latest music    

eric anasema kuwa aliamua kuwaalikia wsanii mbalimbali katika moja ya matamsha makubwa aliyoamua kufanya tandale na kwa sababu aliamini kuwa diamond ametokea huko basi tamasha linaweza kuwa lenye mafanikio kwa sababu lengo lilikuwa ni kuwarudishia maskini fadhila na kuwa nao karibu.

Eric anasema kuwa kutokana na uongozi wake unaomshauri sana Diamond wamekuwa wakimshauri sana kufanya shoo nje ya nchi kuliko za humu ndani bila kujali kuwa kuna watu wengi sana wanaompenda msanii huyo nchini na hata kufikia kuiga baadhi ya vitu vyake kama kutengeneza nywele na kuvaa mashati yenye jina lake.

Hata hivyo Eric aanasema baada ya kuyaona hayo yote, aliamua kundika makala ya kumhusu diamond huku akitaka kumshauri kwa baadhi ya mambo kama hayo lakini cha ajabu viongozi wake akiwemo Babu tale aliamua kumchambua sana Eric na mpaka akuhojiwa katika kipindi cha shilawadu huku akiogea maneno yasiyo na busara kumhusu.

Hata hivyo Eric anasema kuwa baada ya hapo hakupata kuwasiliana tena na WCB mpaka wiki iliyopita alipopigiwa simu na Babu tale tena akimtaka kuhudhuria tukio ambalo siku zote yeye amaekuwa akiomba wasanii walifanye na ndo maana hata hakukataa kwa sababu aliamini ni jambo muhimu.

Kwa kumalizia Eric anaona kuwa alichokifanya Diamond ni kitu chema na ameona jinsi gani wasanii wamekuwa na faida kubwa katika jamii inayowazunguka ,

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.