Loading...

Esma Afungukia Maisha Baada Ya Kuachwa

February 01, 2019 at 09:21
Esma Afungukia Maisha Baada Ya Kuachwa

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kuongelea maisha yake Baada ya kuachwa na aliyekuwa mume Wake Petit Man.

Esma amefunguka na kusema kuachika kwake kwenye ndoa hakujamfanya akate  tamaa ya kuendelea na maisha mengine ya kawaida.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Esma ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuna wanawawake wengine wakiachwa huwa wanakuwa kama wamepatwa na ugonjwa wa kuwafanya washindwe kufanya chochote maishani wakiwaza tu mapenzi, jambo ambalo halipaswi kufanywa na mwanamke anayejitambua.

Ukweli ni kwamba kuachika kwangu hakujanifanya nishindwe kuendelea na maisha yangu ya kujitafutia riziki. Kwanza nilipoachwa ndiyo maisha yakaninyookea“.

Esma alikuwa amefunga ndoa na Petit kwa miaka kadhaa kabla ya kuachana mapema mwaka jana Baada tetesi kusikika kuwa Petit alikuwa amempa mimba mwanamke mwingine.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…